by the way, its Very Long!!!
Maisha yako kama matembezi
mbele unaenda kukaa hauwezi
Somo unapata lakini hufundiki
na hukumbuki
wala huandiki
Matendo yako ni kama sinema ya kutisha
tunaficha macho yetu lakini bado unatusikitisha
Makucha ni marefu tukisogea unaficha
Kesho si mbali naamini tutafika
lakini fikiria hili
weka kwenya akili
utafikaje mbele ukipiga hatua ya pili
unarudi zingine mbili
Ina maana huwazi?
Ndugu hufikiri?
Au ukituona sisi
unaona kama ni siri?
Hamna siri ya watatu wala wawili…
Siri ambayo waweza kuienzi
ni kati yako na Mwenyezi
Maneno yako ni ya mdomo
unaongea bila somo
Waongeaji tunaongea kwa moyo
si kwa ulimi
si kwamba kuonesha Ati mimi
Ati mimi zaidi ya wewe
Nimekubalika Zaidi ya wewe
Umekabilika na nyani?Umekubalika na Mwewe?
Nani kakubali?
Nani kaamka usiku kukutakia hali
Asubuhi akakuongoza safari?
akakusindikiza mpaka huko mbali?
Ni nani kakukubali?
Tatizo ni binadamu sisi
Sio kama sisimizi
wakipata hawaulizi
wataitana wote kama simulizi
beba, safari, tukagawane mbili hizi
Sawa ati na Tushikamane
tukikosewa na tuandamane
lakini lazima Fulani atatoka
atasimulia ataenda kufoka
ni maisha gani bila ushikamano
bila ufikiriaji mapambano
si mapambano ya ushambuliaji
mapambano yale ya ufikiriaji
Kwanini ufanye maamuzi kwa mawazo ya wengine
wakati akili tumepewa kila mmoja, pengine,
labda unahitaji mshauri
unahitaji haya mawazo, unahitaji Kauli
unahitaji chakula lakini kikiletwa hauli.
Sasa ni nini unaomba chakula basi?
Uandaaji ni wa kazi
Lakini wewe unaona sawa
unaona eti..wapumbavu hawa.
Ndio wapumbavu sisi, jina umetupa
Tusioridhika mabaki, mifupa
lakini kumbuka kwamba sisi wanyama
tukikosa chakula wenyewe kwa wenyewe tulana.
ukitembea basi, ukifika huko basi angalia nyuma
haya matoroli tunayoyasukuma
Nyumbani mama ana homa
Mtoto shule anataka kusoma
mali tunayo
lakini kama ya kwao
kuenda haiendeki
tukitenda halipendeki
na tufanye nini utufurahie
utafanyie utufikirie?
Umekaa kwenye kochi,
nne yako haitoshi
piga basi na tano
kwasababu sisi hatuwezi maandamano
Lakini kumbuka kila mwisho wa mwezi
Maisha yako kama matembezi
Mbele unaenda kuendelea huwezi.
No comments:
Post a Comment