Wednesday, December 8, 2010

Happy Independence Tanzania!!

Leo Tanzania Inatimiza.. Miaka 49 Ya Uhuru... Happy Independence My Beloved Tanzania...
Ruka basi Kama Mmasai!


Cheza Basi hata ka-Tumogele
Jipongeze na moja baridi...moja moto...



Ningekuwa Nyumbani siku kama hii ni TV na mimi!..nyumba Nzima tunaamka Asubuhi kuangalia Maadhimisho ya uhuru Uwanja wa Taifa...Kama ni pilau twende..na soda juu...Lakini Leo..hapa nilipo ni chuo na Mitihani, siyo hata Sikukuu!Yani najisikia kama kitu hikjakamilika!. ..lakini baadaye nitajumuika na WaTanzania Wenzangu Kusherekea Siku hii...


Tusherekee Kwa Amani  kama WaTanzania wa kweli maana kwa Ninanvyoona popote napokwenda WaTanzania ni Watu Wa amani na wakarimu. Lakini...Huu Uhuru tunaousherekea..Tunautumia? Tunaufaidi? Tunaundeleza? Au bado Tunachungulia? ..Fikiria..Tumia Uhuru wako Ipasavyo.... Si Kwa Uhalifu na Matendo ya kuturudisha nyuma zaidi ya siku za uhuru jamani! Loh!  Hata na miaka 49 tuliyonayo...bado ni watoto mbele ya Mataifa mengine...Tunahitaji kukua zaidi, kuendelea zaidi na sisi tu na  si watu wengine ku-leta hayo maendelo na huo ukuaji. Ukuaji sio Mijini tu, Ni Tanzania kama Tanzania..miji hata Vijiji 
Again...Happy Independence Guys!! 

No comments:

Post a Comment