Nchi zote za Afrika zilipata uhuru kutoka katika nchi za Magharibi baada ya kutawaliwa, lakini hali inaendelea kujirudia kama enzi za ukoloni.
Hayati Mwalimu Julius Nyerere alilielewa hili na alijaribu kutuelimisha kwa kusema “Jambo lolote linalokuongezea uhuru ni jambo la maendeleo, hata kama halikuongezei shibe,” kwa maneno mengine maendeleo hayatokani na shibe bali yanatokana na uhuru.
Hapa naweza kusema kuwa uhuru ni hali ya kiakili na hisia, basi maendeleo yote yanatokana na akili na hisia.
Kwa kawaida mtu anakuwa huru iwapo tu anathamini uhuru wake na kujituma kuhakikisha uhuru wake unatumika vizuri katika maamuzi na utendaji bila kutegemea watu wengine ili kulinda uhai wake.
Kwa mtazamo huo utaona kwamba Mwalimu Nyerere alikuwa mbele sana kimawazo kuliko viongozi wengi duniani.
Sina shaka wenzetu wa nchi za Magharibi na viongozi wa nchi hizo walimwelewa vizuri na ndiyo maana mashambulizi yalielekezwa kwake binafsi pamoja na mawazo yake kwa lengo la kuyavuruga ili yasilete matunda.
Kuna umuhimu wa kutoka nje kidogo kuangalia juhudi za Mwalimu Nyerere za kulinda uhuru wa Tanzania na mashambulizi aliyoyapata yakiwa na nia ya kuvuruga juhudi zake.
Katika sera ya Ujamaa na Kujitegemea, haikuwa itikadi ya kisiasa kama ilivyokuwa ikichukuliwa na nchi za Magharibi, bali ilikuwa ni mfumo wa maisha ya viumbe kama binadamu vinavyoishi kwa uhuru wake.
Waingereza iliwachukua zaidi ya miaka 300 kuelewa maana ya uhuru, lakini Mwalimu aliweza kulielewa hili katika miaka mitano ya uhuru; na baadaye asilimia kubwa ya viongozi duniani walioelewa maana ya maneno yake kuhusu uhuru walishtushwa kwa kiwango kikubwa, hii ni kutokana na tabia ya binadamu ya kupigania rasilimali bila kujali au kuthamini uhuru.
Kitendo cha kuyapa mawazo yake jina la itikadi ya kisiasa kilibadilisha maana ya ujamaa na kujitegemea, hii ni kutokana na kuwa mawazo yoyote yanayoitwa itikadi ya kisiasa yana mawazo mbadala yanayoweza kufanya kazi kwa kiwango cha chini.
Mawazo ya ujamaa na kujitegemea yalikuwa na lengo la kuweka mfumo wa maisha katika hali ya kujitegemea ili kuongeza uhuru wa maamuzi ya kujitegemea kwa jamii, jambo ambalo halikufanikiwa kwa kiasi kikubwa na hii ni kutokana na mtazamo wa mataifa ya Magharibi kupunguza nguvu za kujitegemea kama taifa huru.
Kwa mantiki hii, unaweza kutengeneza mazingira yanayoonyesha watu ambao baada ya kutawaliwa na kuvurugwa akili wanaona kuwa kupitia madirishani wanapoingia nyumbani ni jambo la kawaida.
Lakini akatokea mjanja akasema kuwa jambo sahihi ni kupitia mlangoni na si dirishani, kama hutaki waelewe hili na unataka waendelee kupitia madilishani jambo jepesi ni kuwaeleza kuwa hilo alilosema ni itikadi ya kisiasa, hivyo ndivyo wawekezaji wanavyoingia kuchukua rasilimali yetu.
Kwa kutumia mbinu hii viongozi wa Tanzania wamerudishwa usingizini na hawaelewi tena maana ya uhuru na nina wasiwasi hawataamka tena.
Mwalimu Nyerere alibaini kuwa uhuru ni kuishi kama jamii moja kwa kujitegemea, ikiwa na dhumuni la kulinda uhai wa watu wote, hii ina maana kuwa rasilimali za nchi zitumike kulinda na kudumisha uhai wa Waafrika kama vile ndugu.
Mfano Marekani wao wamekuwa wanalinda rasilimali yao ya mafuta tangu miaka ya 1900, ambapo Canada, Israel na Japan wao wanajitegemea katika maamuzi na vitendo ili kulinda uhuru wa taifa.
Hii ipo tofauti sana na nchi ya Tanzania kwa mfano viongozi husema kutegemea misaada kunatishia uhuru wetu, hii si sahihi kwa sababu tunaowaomba misaada ndio wanaokimbilia nchini kwetu kuwekeza na jambo jingine wanaeleza matokeo ya tatizo badala ya chanzo cha tatizo.
Huku ni kufungwa kamba kiakili, kitendo cha kutegemea misaada kwa asilimia zaidi ya 40 ni sawa na kitendo cha kuomba hali inayodhihirisha kuwa tayari tumepoteza uhuru.

By Samwel Mtuwa
Freemedia.co.tz
Baadhi ya mawazo ya watu kuhusu uhuru
What Independence z Celebrated 2day? Kwani Wazungu Walitutesa zaidi ya Mateso ya Serikali ya Independent Tanzania....???
Albert M Valentine: naona kwa miaka 49 tunajaribu kuendelea lakini bado, tumeendelea lakini katika mwendo wa taratibu sana.
Richard Joshua,In dis 49 yearz nat much has developd wat we can b proud of is da peace n lov dat hav 4 ol dis tym
Misonge Silanda,Miaka 49 ya uhuru kwa mtazamo wangu Tanzania bara imepiga hatua ukizingatia bado ni nchi Changa,Amani na Usalama kwa kiasi kikubwa tumejitahidi kulinda,Kielimu na ata kisiasa watanzania Bara wengi wamefunguka na kujitambua!! Tuzidi kujituma sote somedays Tutafika mbali sana!

!

No comments:
Post a Comment