Nimeshawahi kujadili hili swala kwamba eti Kiswahili hakijitoshelezi...na mimi ni mmoja wale wabishi ambao kila siku tukiwa kwenye huu mjadala nasema NDIO na ninabisha kwa moyo wote. Kiswahili kimekopa maneno mengi sana kutoka kwenye Kingereza na kuna maneno mengina ambayo piga ua hayana 'Swahili Translation' hizo ndo kila siku ndo mada zangu kuu, Ray the Greatest (Muigizaji) Vincent Kigosi alikuwa kwenye kipindi Fulani cha filamu akisema kua Ndio Kiswahili hakijitoshelezi ndo maana wanatumia hayo majina wanyotumia kwenye filamu..jamani...Oprah, Beyonce, Duh! Hii ni Baada ya BODI ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza kutangaza kwamba kuanzia sasa ile tabia iliyozoeleka ya kutumia majina ya Kiingereza katika filamu za nyumbani si ruhusa na hairuhusiwi kabisa. Wanataka kusikia Chausiku..Mwanahawa, Mwantumu, Joisi..ha ha..Ray Akasema
“Lugha yetu ya Kiswahili hajitosherezi ndiyo maana tunatumia majina ya Kiingereza, najua wataalamu wa Kiswahili wanaweza kukataa kuhusu hilo” Haya yalikuwa ni maneno ya Ray, lakini aliongezwa swali na bibie huyu aliyekuwa makini kweli kweli
“Pamoja na hayo lakini bado sipendwezwi na hata matumizi ya lughahii”
Akatolea mfano katika picha moja ya hapa hapa Bongo kuwa kuna mtu alisikika akiongea maneno ya Kiingereza ambayo hayakuwa sahihi nalo anasemaje?
“Lugha hii siyo yetu ndio maana hata The Great alivyoenda Afrika ya kusini walisema sana ooh hajui Kiingereza, lakini hapa alikuja Rais wa nchi ya China hajui Kiingereza lakini hakuna mtu aliyesema ikumbukwe ile si Lugha yetu ndio maana makosa kama hayo yanatokea”
Kwasababu ya mada husika imenibidi niandike kwa Kiswahili...
Anna M.
No comments:
Post a Comment