Sunday, April 3, 2011

From Harusi Trade Fair

Kutoka  Harusi Trade Fair.. ambayo ilifanyika tarehe 1-3 April


Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia na watoto, Mh. Ummy Ally Mwalim, jana alipata muda wa kutembelea maonyesho yanayoendelea ya Harusi ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee juzi jioni.
Akizungumza baada ya kutembelea mabanda yote yanayokadiriwa kuwa zaidi  ya 50 ya wajasiriamali tofauti tofauti wanaojihusisha na masuala ya harusi, Naibu waziri alimsifu muaandaaji wa maonyesho hayo, ambae pia ni mbunifu mahiri wa mavazi nchini, Mustafa Hassanali kuwa ni mjasiriamali anayejituma na ni mfano wa kuigwa.
“kwa kweli Mustafa amefanya kitu cha kipekee sana, naa ni mfano wa kuigwa, hii inawapa wafanyabiashara husussani wale wa mapabo na keki kuweza kujitangaza na kujifunza mengi wao kwa wao” alisema mheshimiwa Waziri.

“mwaka huu sambamba na maonyesho haya, tumeweza pia kuzindua jarida ambalo ni mahususi kwa masuala ya Harusi, hii ni kwa mara ya kwanza Tanzania kuwa na jarida la namna hii ambalo litatoka mara nne kwa mwaka, pia tumeweza kuwa na midahalo mbalimbali ya wazi ya kuelimisha juu ya masuala ya Harusi na ndoa” alisema Hassanali.
Mustafa Hassanali talks to Minister of State in the Prime Minister's Office (Policy, Coordination and Parliamentary Affairs) William Lukuvi during HARUSI TRADE FAIR 2011 visit at Diamond Jubilee Hall
Im hearing there were Zanzibar Harusi Packages...for weddings in Zanzibar...exotic!

No comments:

Post a Comment