Saturday, April 9, 2011

Balozi Akutana Na WaTanzania Reading

URBAN PULSE CREATIVE inapenda kuwaleta video fupi ya ziara maalum ya Mh Balozi wetu Peter Kallaghe kuhusu mpango mzima wa ziara yake ikiwa ni mara yake ya kwanza kufika katika mji wa Reading hapa UK na kukutana na watanzania. Kwa mujibu wa ratiba yake leo Mh Ataanza kukutana na wafanya biashara pamoja na wajasilimali, vikundi  mbalimbali vya kitanzania ili kujenga mahusiano mazuri  ya karibu baina ya ubalozi na watanzania waishio hapa nchini uingereza ikiwa ni  pamoja na kusikiliza matatizo yao na kutoa ushauri jinsi gani ya kukabiliana nayo pia kujua msimamo halisi wa kiserikali wa kuwasaidia watanzania waishio ughaibuni.

kushoto Frank, Mh Balozi na Nocha katika picha ya pamoja
Pia URBAN PULSE inawaletea matukio katika picha kuhusia na ziara Maalum ya ,Mh Balozi Peter Kallaghe pamoja na mkewe mama Balozi walioambata na mjumbe toka ubalozini ambaye ni second secretary Allen Kuzilwa. Baada ya kuwasili mjini Reading Mh balozi alipata fursa ya kukutana na watanzania mbalimbali pia kufanya majadiliano ya kina kuhusu changamoto mbalimbali zinazo watokea na jinsi gani ya kuzikabili kwa ufasaha zaidi...
(More Images After the Break)

Kikao Kinandelea

 kushoto Said Surur anaewakilisha TA London akimhabarisha Second Secretary Allen Kuzilwa kutoka Ubalozini aliaambatana na Balozi katika ziara hii

Mh Balozi akiongea na Baadhi ya wafanya biashara na wajasimali katika mji wa Reading

Mh Balozi akitoa ufafanuzi kwa wadau kuhusiana na mambo mbalimbali, pembeni yake akiwa na mama Balozi Mrs Joyce Kallaghe pamoja na mama Maria wakifuatilia mada hiyo kwa makini

Mh Balozi alieambatana na mama Balozi wakiwa na Viongozi wa TA pamoja na crew ya urban Pulse

Mh Balozi Kallaghe akijibu Moja ya Hoja nzito zitizolewa na wadau
Mjasilimali Ben Chisumo Kutoka Locas Impex akitoa dukuduku lake kwa Mh Balozi.


Mjasilimali Ben Chisumo Kutoka Locas Impex akitoa dukuduku lake kwa Mh Balozi
Info Credits: Frank Eyembe, Uban Pulse

No comments:

Post a Comment